Mapenzi ni kidonda ukiwaza utakonda. Harmonize ameonyesha bado
anamhitaji Jacquline Wolper kwenye himaya ya moyo wake baada ya kupigwa
kibuti.
Baada ya kusambaa kwa taarifa kuwa wawili hao wamemwagana tena huku
Wolper akipigilia msumari kuwa jambo hilo ni ukweli mtupu japo Harmo
alikuwa akilificha, sasa muimbaji huyo ameanza kuonyesha kuwa jambo hilo
ni kweli.
Harmonize ameonekana katika kipande cha video alichokiweka Wolper katika
mtandao wake wa Instagram akimuimbia mpenzi wake huyo wa zamani wimbo
wa ‘Ibaki Stori’ wa Rich Mavoko kama njia ya kumshawishi mrembo huyo
asahau yaliyopita.

Please do not enter any spam link in comment box